August 2, 2011

Welcome on board

Lets welcome on board new Blogger Kijakazi Yunus with her afrokijah blog

 Habari ya siku tele kaka, natumai unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku.. Napenda kukujulisha kuwa nina blog yangu ambayo inaitwa afrokija, inayozungumzia hasa masuala ya muziki na wanamuziki Barani Afrika na  ninalenga hasa yale yanayojiri kwenye kipindi changu cha Afrobeat kinachorushwa na East Africa TV kila jumamosi saa 1 jioni, ingawa pia napost na habari zingine zinazonigusa ambazo naamini watu wengine wangependa kuzifahamu. Hivyo naomba uwafahamishe wapenzi wa blog yako kuwa kuna hii blog ili waweze kupata habari za wanamuziki wa Afrika kupitia blog yangu(afrokija)

Natumai utanipa ushirikiano
Nakutakia kazi njema.
 Ramadhani Kareem.

UPUUUZI HUU WA WAZOA TAKA KIMARA B SALANGA UKOMESHWE!

Yapata miezi kadhaa sasa baadhi wakazi wa maoeneo ya Kimara B kata ya Salanga Jimbo la Ubungo wamekuwa wakiamka asubui na kukutana na marundo ya taka barabarani karibu kabisa na nyumba zao. 


Mwanzoni ilidhaniwa kwamba labda kuna gari la taka liliharibika na hivyo taka hizo kudondoka hapo, lakini kwa kitambo sasa imekuwa ni kama kawaida ni kama vile wazoa taka wa eneo hili wameamua kwa makusudi kubadilisha baadhi ya maeneo kuwa dampo, cha ajabu ni kuwa wanatupa taka hizo alfajiri kabla wakazi wa eneo husika kuamka ama kuwa wameshatoka. 

Baada ya kuchunguza kwa kitambo kidogo imegundulika kuwa wazoa taka hao wanafanya hivyo kwa makusudi katika zile nyumba ambazo hawapati ushuru wa taka kutokana na kuwa hakuna taka za kuzoa humo, nyumba hizi nyingi zina maeneo makubwa kiasi cha wenyewe kuchimba mashimo ya taka ndani ya fensi zao na wengine kutumia taka hizo kama mbolea, kitendo hiki ndicho kinapelekea wazoa taka wa Mtaa wa Salanga kuamua kwa makusudi kuchafua maeneo hayo kwa malengo binafsi kama picha hii inavyoonesha. 

Wakazi wa nyumba hii wameamka asubui na kukuta taka toka sehemu tofauti tofauti zimetupwa mbele ya geti lao, hii haiingii akilini, tunawaomba Viongozi husika wa maeneo haya kuanzia Mwenyekiti wa mtaa na diwani kupitia kwa Mbunge wa Jimbo John Mnyika kuongea na watu hawa na kukomesha vitendo hivi ambavyo si tu ni vya kipuuzi bali vya kishenzi pia. 

Wakazi wa Kimara B, Salanga. 

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...